KULEA VIFARANGA
Utangulizi
Kwa kawaida au katika hali
halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea
vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa
zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na
kukosa uangalizi wa karibu. Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba
yenye joto, chakula kinachofaa na maji safi , kuwakinga dhidi ya magonjwa
masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni
yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao hatimaye hutoa mazao mengi
yanayompa faida. Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga
vifaranga wake kwa muda mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku
kurudia kutaga na hivyo kupata vifaranga wachache zaidi kwa mwaka. Lakini
vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema, kama majuma matano hivi baada ya
kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga mapema na idadi ya kuku kwa
mfugaji huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi. Mwongozo huu unaeleza jinsi
ya kufuga vifaranga vizuri ili hatimaye mfugaji apate faida zaidi.
Nyumba ya
kulelea Vifaranga
Ukipenda kujenga nyumba ya
vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a Nyumba ya vifaranga iwe karibu
na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
b) Ijengwe hatua 20 au zaidi
mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya
maambukizi ya magonjwa.
c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu
ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na
mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha
ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
e) Ijengwe kwenye sehemu
isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii
husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.
Ukubwa wa Nyumba
Eneo:
Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika
muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta
za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye meta 10 za mraba
inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye
eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25.
Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi
na uwape vifaranga eneo la kuwatosha.
Sakafu:
Sakafu nzuri katika nyumba ya
vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti iliochanganywa na zege. Ili
kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kirahisi
katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza
kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.
Ukuta:
Ingefaa kuta za nyumba za kulea
vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe. Kuta za matofari na udongo
zipigwe lipu ili kurahisisha usafi shaji wa nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu
wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9
– 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu
iliyobakia yenye meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.
Mbao:
Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya
mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni
vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea na wadudu.
Madirisha:
Unaweza kutumia maboksi, mikeka
ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa
misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao
ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa
kutosha katika nyumba ya vifaranga.
Paa:
Mjengo wa paa uwe unaoweza
kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na tundu la kutoa nje hewa
yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe, mabati, makuti au
nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe
bila kuchelewa.
Vyombo kwenye
nyumba ya vifaranga
Kuna vyombo vingi pia njia nyingi
zinazotumika katika kulea vifaranga kutegemeana na hali halisi ya mfugaji.
Mfugaji kijijini anaweza kutumia vyombo vifuatavyo:
1. Vitalu
Vifaranga hutunzwa ndani ya
kitalu kilichotengenezwa kwa mbao au karatasi ngumu zinazotumika kujengea dari.
Au katika mazingira ya kijijini unaweza kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia.
Upana wake uwiane na wingi wa vifaranga ulionao na kina chake kama mita moja.
Ukuta wake uwe na tabaka mbili za magunia hayo zilizoachana kwa nafasi ya inchi
tatu au nne. Katikati ya nafasi hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za mpunga.
Tayari utakuwa umepata kitalu cha kulelea vifaranga.
Ndani ya kitalu weka taa ya
chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.
2. Taa ya chemli
(taa ya mkono)
Kutegemeana na hali ya hewa taa
moja ya chemli inaweza kulea vifaranga 50 au zaidi. Hakikisha kuwa unayo akiba
ya mafuta ya taa ya kutosha, vioo, utambi n.k. Taa moja hutumia debe moja la
mafuta ya taa kwa muda wa siku 16 hadi 20. Unashauriwa uweke mafuta kwenye taa
asubuhi na kukagua jioni kama yanatosha kwa sababu taa ikizimika
usiku utapata hasara ya vifo kwa
vifaranga kujikusanya na kukosa hewa .Weka mafuta ya
kutosha lakini usijaze taa. Joto
la taa za chemli hurekebisha kwa kupandisha au kushusha utambi pia kuongeza au
kupunguza idadi ya taa.
3. Jiko la Mkaa
Jiko la mkaa linaweza kutumika
badala ya taa kwa ajili ya kuwapa vifaranga joto. Unapotumia jiko la mkaa ni hakikisha
kwamba mkaa unaotumia hautoi moshi na chumba kinapitisha hewa safi na ya
kutosha. Pia jiko liwekwe juu ya matofaili ili kuzuia vifaranga wasiliguse.
4. Mwamvuli
Mfugaji akimudu anaweza
kutengeneza mwamvuli wa kuning’inia juu ya kitalu cha kulea vifaranga kwa
kutumia makaratasi magumu ya “hardboard”. Mwamvuli unasaidia kupunguzaupotevu
wa joto na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya taa. Kwenye mwamvuli wa duara
toboa tundu moja ili kupitisha hewa yenye joto. Angalia mviringo wa mwamvuli
wako uwiane na ukubwa wa kitalu chako. Ili kuwapa vifaranga uhuru wa kufuata au
kuepuka joto. Ni lazima mwamvuli uwekwe juu ya matofali na kila juma inabidi
uinuliwe juu kiasi cha cm 5 (inchi 2, kufuatana na hali ya hewa.
5. Vyombo vya
chakula (Vihori)
Ili vifaranga
wakue vizuri vyombo vya chakula lazima viwafae. Vipimo pamoja na idadi ya
vyombo vya chakula ni vya muhimu viwatosheleze. Chombo chenye urefu wa (futi 3
x inch 3) kinatosha vifaranga 100. Ukitumia mbao kutengeneza vyombo vya chakula
unashauriwa mbao ziwe unene wa cm 1/25 (inchi ½). Pia, unaweza kutumia sahani
za kawaida unazotumia nyumbani kuwawekea vifaranga chakula. Chombo cha kulishia
vifaranga
6. Vyombo vya
maji:
Chombo chochote chenye kina
kifupi kinafaa kwa kuwayweshea kuku ila budi kiinuliwe ili vifaranga wasiweze
kuingiza takataka za chini kwenye maji. Pia kama ni cha wazi maji yawekewe
changarawe safi kabisa ili kuzuia vifaranga wasiloane maji. Au tumia sahani na
makopokama ifuatavyo. Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza maji
katika kopo halafu lifunike kwa sahani na ligeuze. Kinywesheo cha vifaranga
Maandalizi kabla
na matunzo baada ya kupokea vifaranga
Maandalizi kabla
ya kupokea vifaranga
Inashauriwa vifaranga walelewe
katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne. Chumba kitayarishwe siku kumi
na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo:
• Matundu yote yaliyo kwenye
sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe.
• Kama chumba hicho kina sakafu
ya saruji, kisafi shwe kwa maji ya moto na baadaye kinyunyizie dawa kama vile
Rhino au Dettol ya kuua wadudu. Ikiwa chumba hicho hakina sakafu ya saruji, toa
takataka zote kisha mwagia chokaa au majivu.
• Mazingira ya nje ya banda
yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. Kusafi shwe hadi
kufi kia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda.
• Katika chu na umbile la duara, itengenezwe kwakutumia
karatasi ngumu au majamvi. Mduara huhifadhi joto, huzuia upepo na huzuia vifaranga
wasiende mbali na chanzo cha joto.
• Sakafu iwekwe matandazo
yaliyopigwa dawa mfano ya kuuwa wadudu kama Municipal disinfectant. Matandazo
yaweza kuwa pumba ya mpunga, maranda ya mbao, nyasi, mchanga, maganda ya
karanga n.k. Masaa mawili kabla ya kuwasili vifaranga vyenye umri wa siku moja
taa au jiko liwashwe kwenye chumba cha kulelea vifaranga. Hii itasaidia ili
maji na chumba kuanza kupata joto la kutosha kuwawezesha vifaranga kula, kunywa
bila shida. Baada ya masaa mawili kupita ndipo chakula kianze kuwekwa kwenye
vyombo vya chakulana vifaranga waanze kula.
Matunzo baada ya
kupokea vifaranga Kuwapa joto
Mfugaji anaweza
kulea vifaranga wengi kwa kutumia Kitalu (mduara) unaoweza kutengenezwa
Mfano wa brooder kwaajili ya kutunzia
vifaranga
Kama joto halitoshelezi utaona yafuatayo
Vifaranga
wakiona baridi , hujikusanya karibu zaidi na chanzo cha joto. au wao wenyewe hujikusanya
pamoja kwenye pembe ya kitalu au nyumba na hulia kwa sauti. Ukiona hivi ongeza kiwango
cha joto adi waonekane kutawanyika kote kitaluni.
Katika mduara/
kitalu cha kulea vifaranga mfugaji anatakiwa kufuatilia na kutambua kama hali
ya joto iliyopo inawafaa vifaranga au la. Ufuatiliaji wa karibu utamsaidia
kuchukua hatua mapema endapo marekebisho yatahitajika. Hii utafahamu kwa
kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya kitalu .
Kama joto linatosheleza utaona
yafuatayo
• Vifaranga vitalia kwa furaha,
• Vitakimbia kimbia,
• Vitakunywa maji,
• Vitachaguachagua takataka na
• Kuonyesha shughuli nyingi, zote
hizi ni dalili nzuri kuwa joto linatosha.
Mfano wa kitunza joto kwa
vifaranga
Kama joto
likizidi utaona yafuatayo
• Vifaranga wakikaa mbali na
vifaa vya joto nidalili kuwa joto limezidi.
• Joto likiwa kali vifaranga
hukimbia kutoka kwenye mwamvuli (kama umewekwa).
• Husinzia na huzubaa. Katika
hali hii itabidi upunguze joto kwa kupandisha taa juu na kama bado joto ni kali
punguza vifaa vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi ya kunywa.
Kama kutakuwa na
upepo unaopuliza kutoka upande mmoja utaona yafuatayo
Vifaranga
watajikusanya upande mmoja wa kitalu mbali na upepo unakotokea. Kutegemeana na
jinsi utakavyowaona vifaranga wanafanya, kama wataashiria tatizo, fanya marekebisho
mapema kabla hayajatokea madhara kwa vifaranga.
Katika majuma 5
ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na
katika majuma 3
yanayofuata joto hujitajiwa wakati wa usiku tu.
Hata hivyo
ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kufuata maeneo
tofauti na pia kutegemeana na majira tofauti ya mwaka. Hivyo kama hali ya
baridi ikizidi, muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto kali taa zinaweza
kuzimishwa hata kama ni juma la kwanza au la pili. Jambo la msingi ni mfugaji
kuwa macho na kuwapa vifaranga joto la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika
kuwa ya baridi ghafla.
Hali ya hewa ikiwa nzuri
madirisha yafunguliwe katika juma la kwanza au la pili kwa ajili ya kutunza
matandazo sakafuni yasiwe na unyevu. Vifaranga huota manyoya mapya wakiwa na
umri wa majuma 5 – 6 lakini huotesha manyoya ya kutosha katika juma la 8.
Wakiisha ota manyoya ya kutosha vifaranga wanaweza kuvumilia zaidi hali ya
baridi. Ufuatiliaji wa karibu ni muhimu kwa kipindi chote cha majuma matano (5)
ili kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima.
Waondoe
vifaranga kwenye kitalu cha kuwalea mara tu wakiwa na manyoya ya kutosha, yaani
katika juma la 4 -5 kutegemeana na hali yao ya manyoya na hali ya hewa iliyopo.
Ulishaji wa
Vifaranga
Chakula na Maji
Ili vifaranga
wawe na maendeleo mazuri ya ukuaji, wanatakiwa wapewe chakula chenye virutubisho
vyote vinavyohitajika mwilini ambavyo ni Protini, Madini, Wanga na Vitamin pamoja
na maji safi wakati wote.
• Pia chakula kunaweza
kuchanganywa na mchanga kidogo ambao husaidia usagishaji wa chakula
kilicholiwa.
• Hakikisha vyombo vya maji
vinakuwa safi wakati wote.
• Chakula na maji yabadilishwe
kila baada ya masaa 24.
• Hakikisha vifaranga wanapewa
chakula wanachoweza kumaliza katika masaa 24 ili kuzuia uharibifu. Siku 7 – 10
baada ya kupokea vifaranga vyombo vya mwanzo vya maji na chakula vibadilishwe
wawekewevyombo vya kawaida. Vifaranga wapewe maji safi , vyombo vya maji visafi
shwe na kujazwa maji mara mbili kila siku. Kila asubuhi sehemu zilizo na vyombo
vya maji zikaguliwe na takataka zenye unyevu ziondolewe.
Vyombo vya chakula vijazwe nusu
hasa vifaranga wakiwa na umri wa siku 10 – 14. Pia vifaranga wakiwa na umri huo
huo wapewe majani mabichi yaliyo bora na yenye thamani. Majani yafungwe mafungu
na kuning’inizwa kwa kamba.
Vyombo vya
chakula na maji
Vyombo vya
chakula na maji vinaweza kuwa ni makopo, sufuria, karai n.k. Pia vinaweza kuundwa
kwa kukata madebe, galoni za plastiki, vibuyu n.k. Aidha vyombo hivyo vinaweza
kutengenezwa kwa kutumia mbao, mianzi, Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa vyombo
hivyo haviruhusu kuku kuchafua chakula au maji. Mfano wa vyombo vya chakula na
maji ambavyo mfugaji anaweza kujitengenezea.Mfano wa kilishio Vifaranga wakiwa
bado wadogo anaweza kutumia sahani za chakula kuweka kokoto safi na
kuzitumia kunyweshea vifaranga
maji.
Aina ya vyakula
Kiasi
( Kilo)
Nafaka kama mahindi au mtama 40
Pumba za mtama, mahindi, uwele, 27
Mashudu ya, alizeti, ufuta,
karanga, au soya 20
Unga wa mifupa, chokaa 2.25
Dagaa au mabaki ya samaki 10
Chumvi ya jikoni
0.5
Virutubisho (Premix) 0.25
Jumla 100
Mfano wa
mchanganyiko wa chakula cha vifaranga
Mwavuli:
Kama uliweka
mwavuli kwenye kitalu uinue juu kiasi cha fi ti 1 kila juma. Unaweza kuondoa
mduara vifaranga wakiwa na umri
wa majuma 4 – 5. Lakini mwamvuli usiondolewe mpaka
vifaranga viote manyoya ya
kutosha.
Vichanja:
Vifaranga vipewe vichanja ili
vizoee kupanda na kulala juu, vikiwa na umri wa majuma 4.
Chanjo na tiba
ya Magonjwa
Ni wazi kuwa
hatari kubwa inayokabili vifaranga ni magonjwa. Yapo maradhi mengi ya
vifaranga. Hata hivyo itakuwa
vigumu kuyaelezea maradhi yote hapa. Kitakachoelezwa
katika mwongozo huu ni magonjwa
yanayosumbua mara kwa mara kwenye ukanda wa kati
wa nchi hii. Ukipata shida
tofauti na zinazoelezwa hapa tafadhali mwendee Bwana Mganga
wa mifugo aliye karibu
akusauidie.
Kinga dhidi ya
magonjwa
Ni muhimu sana vifaranga kupewa
kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali yanayotokea katika eneo husika. Kinga
nyingi hutolewa kwa njiaa ya chanjo hasa kwa magonjwa yasiyotibika kama
tutakavyoona katika maelezo yafuatayo.
Chanjo muhimu
kwa vifaranga
Kwa magonjwa yanayosababishwa na
virusi
Ugonjwa Dalili
za Ugonjwa Kinga/Tiba
Mdondo
Ø Vifo vingi vya
ghafla kwenye kundi hadi 90% -100%.
Ø Kizunguzungu,
kupinda shingo, kutembea kinyume nyume, kupooza mabawa,kuanguka chali, kupoteza
fahamu na hatmaye kufa.
Ø Kupoteza fahamu
ya kula, kuzubaa, kusinzia,kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani kibichi na baadaye
kufa.
Ø Hakuna tiba.
Ø Kinga: chanja
kwa kutumia chanjo ya kideri vifaranga wakiwa na umri wa siku tatu na rudia
baada ya wiki tatu na kila baada ya miezi mitatu.
Ø Hakikisha usafi
wa banda na vyombo.
Ø Kutenga
vifaranga wanaoumwa
Ø Tenga vifaranga
wagenikwa muda wa wiki mbili na kuwachanja kabla ya kuwachanganya na vifaranga wenyeji.
Ndui
ya kuku
Ø Vipele vya
mviringo ambavyo huweza kuungana na kusababisha vidonda kwenye upanga, masikio
na miguu hususan sehemu zisizo na manyonya.
Ø Utando mweupe mdomoni.
Ø Vifo hutokea
kwenye vifaranga.
Ø Hakuna tiba
Ø Kinga: wachanje
kuku wakiwa na umri wa miezi miwili kwa kutumia chanjo ya ndui.
Ø Zingatia usafi
wa banda wakati wote.
Ø Watenge kuku
wagonjwa ili wasiwaambukize wengine.Gomboro
Ø Viranga wa umri
wa wiki tatu hadi sita.
Ø Idadi ya kuku
waliopatwa na ugonjwa katika kundi huwa kubwa.
Ø Huharisha
kinyesi cha maji maji.
Ø Hushindwa
kusimama.
Ø Manyoya
husimama, hutetemeka na hatimaye hufa.
Kinga:
Ø
chanja
vifaranga wakiwa na umri wa siku rudia kuchanja baada siku 21.
Tiba ya Magonjwa
kwa vifaranga
Ugonjwa Dalili
za Ugonjwa Kinga/Tiba
Homa ya matumbo(Fowl typhoid), Kuzubaa,
kuvimba viungo vya miguu, kuchechemea, kukosa hamu ya kula, kuharisha kinyesi chenye
rangi ya njano au kijani hatimaye kufa.
Ø Kuku wageni
watengwe na kufanyiwa uchunguzi wa damu kabla ya kuchanganywa kwenye kundi.
Ø Kufanya
uchunguzi wa damu mara kwa mara ili kubaini kuku wenye vimelea vya ugonjwa na
kuwaondoa.
Ugonjwa Dalili
za Ugonjwa Kinga/Tiba
Mdondo Vifo vingi vya ghafla
kwenye kundi hadi 90% -100%.
Ø Kizunguzungu,
kupinda shingo, kutembea kinyume nyume, kupooza mabawa, kuanguka chali,
kupoteza fahamu na hatmaye kufa.
Ø Kupoteza fahamu
ya kula, kuzubaa, kusinzia, kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani kibichi na
baadaye kufa. tiba. chanja kwa kutumia chanjo ya kideri vifaranga wakiwa na
umri wa siku tatu na rudia baada ya wiki tatu na kila baada ya miezi mitatu.
Ø Hakikisha usafi
wa banda na vyombo.
Ø Kutenga
vifaranga wanaoumwa
Ø Tenga vifaranga
wageni kwa muda wa wiki mbili na kuwachanja kabla ya kuwachanganya na vifaranga
wenyeji.
Mafua
kuku (Infectious coryza)
Ø Kutoa machozi.
Ø Kuvimba macho na
hatimaye hutoa usaha wenye harufu mbaya.
Ø Kupiga chafya na
kukohoa.
Ø Kutokwa na ute
kwenye pua na mdomo ambao hatimaye hugeuka na kuwa makamasi mazito.
Ø Kupumua kwa
shida na kutoa saudit ya kukoroma.
Ø Kushindwa kula
Ø Kudhoofika na
hatimaye anaweza kufa.
Tiba:
ugonjwa unatibika kama hatua za kudhibiti zitachukuliwa
mapema. Muone mtaalamu wa mifugo kwa ushauri wa aina ya dawa ya kutumia.
Ugonjwa
unayosababishwa na Protozoa
Ugonjwa Dalili
za Ugonjwa Kinga/Tiba
Kuharisha damu (Coccidiosis)
Ø Kuzubaa
Ø Kushusha mabawa
kama mtu aliyevaa koti.
Ø Kupoteza hamu ya
kula.
Ø Kuharisha
kinyesi chenye rangi ya kahawia au kilichochanganyika nadamu.
Ø Kuharisha damu
Ø Manyoya kutimka
Ø Kupauka kwa
upanga na ndevu
Ø Kudhoofika na
hatimaye huweza kufa.
Tiba:
Ugonjwa huo
unaweza kutibika kwa amprolium, salfa na ESb3 kama hatua za kuudhibiti zitachukuliwa
mapema.Kinga kuepuka unyevunyevu katika matandiko. Kuwatenga kuku
wanaoonyesha dalili za ugonjwa. Kinga
kwa kutumia coccidiostat. Kutibu kwa kufuata ushauri
wa wataalam wa mifugo.
Ø Hushindwa
kusimama.
Ø Manyoya
husimama, hutetemeka na hatimaye hufa
.
Tiba ya Magonjwa
kwa vifaranga
Ugonjwa Dalili
za Ugonjwa Kinga/Tiba
Homa ya matumbo(Fowl
typhoid) Kuzubaa, kuvimba viungo vya miguu, kuchechemea, kukosa hamu ya kula,
kuharisha kinyesi chenye rangi ya njano au kijani hatimaye kufa.
Ø Kuku wageni
watengwe na kufanyiwa uchunguzi wa damu kabla ya kuchanganywa kwenye kundi.
Ø Kufanya
uchunguzi wa damu mara kwa mara ili kubaini kuku wenye vimelea vya ugonjwa na kuwaondoa.
Athari
zinazosababishwa na wadudu wanaonyonya damuKisababishi Dalili za athari za
Wadudu
Kinga/Tiba
Utitiri na viroboto
Ø Kujikuna na kujikung’uta.
Ø Kunyonyoka manyoya,
Ø Kupauka macho, upanga,
ndevu na masikio.
Tiba:
Wadudu wanaweza kudhibitiwa kwa
kunyunyizia dawa kuku walioshambuliwa.
Kinga:
Ø Kuzingatia usafi
wa mabanda ndani na nje.
Ø Kunyunyizia dawa
za kuua wadudu kwenye viota pamoja na kuku anayetaka kuatamia.
Ø Kuchoma au
kufukia mayai ambayo hayakuanguliwa pamoja na maganda ya mayai.
Athari za
Upungufu wa virutubishi kwenye chakula Kisababishi Dalili za athari za Wadudu
Kinga/Tiba
Upungufu wa virutubisho Kudumaa
Tiba:
Athari zinazotokana na upungufu
wa virutubisho zinaweza kurekebishwa kwa kuwapa vifaranga virutubisho vilivyopungua
katika chakula.
Kinga:
Kuwalisha chakula kilicho na mchanganyiko
wenye uwiano sahihi katika wanga, protini, vitamin, madini na maji ya kutosha.
Kumbukumbu ya
kutibu vifaranga kwa kipindi cha wiki 5 tangu kutotolewa
Tarehe Na Mwezi
Ugonjwa Aina na
kiasi cha chanjo Matibabu Gharama Maoni
Kumbukumbu
muhimu wakati wa kukuza vifaranga
Kumbukumbu ya
vifaranga kwa kila Mwezi….. Mei…..
Tarehe Idadi ya vifaranga
Kiasi cha chakula kilichotumiwa
Vifo Vifaranga vilivyo
ondolewa
Vifaranga vya wiki
5
vilivyouzwana
bei yake.
Cypranoanimalfarms.blogspot.com
No comments:
Write comments