UFUGAJI WA NGURUWE
Historia
ya nguruwe
Ufugaji wa nguruwe kwa siku za mwanzo
ulikuwa ukifanyika katika nchi zilizoendelea
kiuchumi. Kitabu chakwanza kinachoelezea ufugaji wa nguruwe na mahitaji yake
kiliandikwa mwaka 1523, na mwandishi wa kitabu hicho alikuwa ni Fitzherbert. Kwa siku za hivi karibuni ufugaji wa nguruwe umekuwa
ukifanyika katika nhi za Afrika. Ongezeko la idadi ya nguruwe duniani
limechangiwa na ongezeko kubwa la watu katika sehemu mbalimbali hapa duniani.
Nguruwe wanaofugwa katka sehemu mbalimbali kwa siku hizi kisayansi
wanaitwa Sus domesticus. Nguruwe hawa wamatokana na makabila mawili ya
nguruwe pori nayo ni nguruwe kabila la Sus
scrofa kutoka kaskazin mwa Ulaya na
kabila linguine ni kabila la Sus procus
kutoka kusini mwa Ulaya, Afrika na Asia.
Muingiliano wa makabila haya ya nguruwe (cross breeding) umepelekea kupatikana
kwa jamii ya nguruwe wanaofugwa kwa wakati huu.
The large white pig breeds |
SABABU ZINAZOPELEKEA FAIDA KATIKA
UFUGAJI WA NGURUWE
- Nguruwe ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kutumia chakula katika kuongeza uzito, nguruwe anauwezo wa kubadili kilo tano- 05 za chakula na kuongeza kilo mija -01 ya uzito wake.
- Nguruwe ni mnyama mwenye uwezo wa kuzaa watoto wengi, ngurwe mmoja anaweza kuzaa watoto 6 hadi 14 mara mbili kwa mwaka.
- Nguruwe ni mnyama mwenye kipindi kifupi cha mzunguko wa uzazi wake, hii ni kwasababu nguruwe hubeba mimba kwa siku 114, pia nguruwe jike huingia joto na kupandishwa akiwa na umri wa miezi saba had inane.
- Nguruwe ni mnyama mwenye kiasi kikubwa cha nyama, hii ni kwasababu asilimia 60% hadi 80% ya mwili wake hutumika kama nyama.
- Nyama ya nguruwe in virutubisho vingi vilevile nyama ya nguruwe inamafuta mengi ambayo huongeza nguvu katika miili ya watumiaji.
- Nguruwe ana uwezo mkubwa watumia mabaki ya vyakula katika ukuaji wake.
- Hakuna ushindani wa aridhi kati ya nguruwe na mimea, hii ni kwasababu nguruwe huhitaji eneo dogo kwa ukuaji wake.
- Nguruwe ni mnyama mwenye uwezo wa kuishi kwenye banda la aina yoyote bila kuathiri ukuaji wake.
- Nguruwe ni mnyama mwe uwezo wa kuishi na kuzoea mazingira mapya bila kuathiri afya na uzalianaji wake.
No comments:
Write comments