Advertisement

Monday, 22 May 2017














WANYAMA WANAOFUGWA KATIKA SHAMBA LA CYPRIANO ANIMAL FARMS
                                     mbuzi katika shamba la CYPRIANO ANIMAL FARMS

Sunday, 29 January 2017

ULEAJI WA VIFARANGA



 
                                              KULEA VIFARANGA

Utangulizi
Kwa kawaida au katika hali halisi, kazi ya kulea vifaranga hufanywa kuku mwenyewe. Hivyo ili kulea vifaranga, mfugaji ni lazima aige kuku anavyofanya. Ikumbukwe kuwa vifaranga husumbuliwa zaidi na hali mbaya ya hewa, magonjwa mbalimbali, kukosa chakula kisichofaa na kukosa uangalizi wa karibu. Ni lazima vifaranga waangaliwe kwa kuwapatia nyumba yenye joto, chakula kinachofaa na maji safi , kuwakinga dhidi ya magonjwa masumbufu kwenye eneo husika na kuwatibu wanapougua. Mfugaji anayefanikiwa ni yule anayelea vifaranga wenye afya nzuri ambao hatimaye hutoa mazao mengi yanayompa faida. Wafugaji wengi vijijini wamezoea kumwachia mama kuku kufuga vifaranga wake kwa muda mrefu hadi wajitegemee. Njia hii humchelewesha kuku kurudia kutaga na hivyo kupata vifaranga wachache zaidi kwa mwaka. Lakini vifaranga vikiondolewa kwa kuku mapema, kama majuma matano hivi baada ya kuanguliwa, na wakatunzwa na mfugaji, kuku hutaga mapema na idadi ya kuku kwa mfugaji huongezeka haraka ndani ya kipindi kifupi. Mwongozo huu unaeleza jinsi ya kufuga vifaranga vizuri ili hatimaye mfugaji apate faida zaidi.

Nyumba ya kulelea Vifaranga
Ukipenda kujenga nyumba ya vifaranga itafaa ufi kirie yafuatayo:-
a Nyumba ya vifaranga iwe karibu na nyumba yako mwenyewe ili uweze kuwakagua vifaranga wako mara kwa mara.
b) Ijengwe hatua 20 au zaidi mbali na nyumba ya kuku wakubwa, hii ni kinga mojawapo ya kupunguza hatari ya maambukizi ya magonjwa.
c) Nyumba ya vifaranga isiruhusu ubaridi au unyevu au wanyama waharibifu kuingia. Lakini nyumba iingize hewa na mwanga wa kutosha kila wakati.
d) Nyumba iwe na eneo la kutosha ili vifaranga wapate nafasi ya kutembea kutafuta chakula na maji bila kubanana.
e) Ijengwe kwenye sehemu isiyoelekea upepo unaotoka kwenye nyumba ya kuku wakubwa. Tahadhari hii husaidia vifaranga kuepukana na magonjwa yanayoenezwa na upepo.

Ukubwa wa Nyumba
Eneo:
 Vifaranga hawahitaji eneo kubwa katika muda wa majuma 4 ya kwanza. Nafasi inayohitajiwa kwa kukadiria ni meta za eneo 1 kwa kila vifaranga 16. Kwa mfano nyumba yenye meta 10 za mraba inatosha kulea vifaranga 160 hadi umri wa majuma 4. Vipimo vya nyumba yenye eneo kama hili inaweza kuwa na hatua 5 kwa hatua 4 au hatua 3 kwa 3.25. Utajenga kutegemea na eneo ulilonalo. Baada ya majuma 4 ya umri ongeza nafasi na uwape vifaranga eneo la kuwatosha.

Sakafu:
Sakafu nzuri katika nyumba ya vifaranga ikiwezekana inafaa ijengwe na simenti iliochanganywa na zege. Ili kupunguza gharama, unaweza kutumia vifaa vya ujenzi vinavyopatikana kirahisi katika eneo lako vitumikavyo kusiriba sakafu kama udongo wa kichuguu au unaweza kulainisha kinyesi cha ng’ombe kwa maji na kusiriba eneo lote la sakafu.
Ukuta:
 Ingefaa kuta za nyumba za kulea vifaranga za matofali, udongo, mabati au debe. Kuta za matofari na udongo zipigwe lipu ili kurahisisha usafi shaji wa nyumba au umwagiaji wa dawa. Urefu wa kuta uwe tangu meta 1.8 – 2.4 (futi 6-8). Sehemu ya kutoka chini ya meta 0.9 – 1.2 (futi 3 – 4) izibwe na ukuta wa tofali au udongo na sehemu ya juu iliyobakia yenye meta 0.9 – 1.2 (futi) 3-4) ijengwe kwa wavu wa chuma au fito.

Mbao:
 Nguzo za miti au mbao zilowekwe dawa ya mbao kama vile “Dudu killer” au oili chafu ili kuzuia kuoza. Ukitumia miti ni vizuri uondoe magome ambayo yanaweza kuweka vimelea na wadudu.

Madirisha:
Unaweza kutumia maboksi, mikeka ya magunia, mapazia ya magunia ni rahisi na yanaweza kuwekwa kwa kupigiliwa misumari kwenye dari na upande wa chini pazia ipigiliwe misumari kwenye ubao ili ininginie.Unaweza kukunja mapazia/magunia ili uingize hewa na mwanga wa kutosha katika nyumba ya vifaranga.

Paa:
Mjengo wa paa uwe unaoweza kuwapatia vifaranga hewa ya kutosha hivyo paa liwe na tundu la kutoa nje hewa yenye joto. Kwa kadri utakavyoweza, unaweza kutumia madebe, mabati, makuti au nyasi n.k. kuezeka nyumba ya vifaranga. Sehemu ya paa ikianza kuvuja iezekwe bila kuchelewa.

Vyombo kwenye nyumba ya vifaranga
Kuna vyombo vingi pia njia nyingi zinazotumika katika kulea vifaranga kutegemeana na hali halisi ya mfugaji. Mfugaji kijijini anaweza kutumia vyombo vifuatavyo:
1. Vitalu
Vifaranga hutunzwa ndani ya kitalu kilichotengenezwa kwa mbao au karatasi ngumu zinazotumika kujengea dari. Au katika mazingira ya kijijini unaweza kutengeneza wigo wa mduara kwa magunia. Upana wake uwiane na wingi wa vifaranga ulionao na kina chake kama mita moja. Ukuta wake uwe na tabaka mbili za magunia hayo zilizoachana kwa nafasi ya inchi tatu au nne. Katikati ya nafasi hiyo jaza maranda ya mbao au pumba za mpunga. Tayari utakuwa umepata kitalu cha kulelea vifaranga.
Ndani ya kitalu weka taa ya chemli ya kutoa joto linalohitajika kwa vifaranga.

2. Taa ya chemli (taa ya mkono)
Kutegemeana na hali ya hewa taa moja ya chemli inaweza kulea vifaranga 50 au zaidi. Hakikisha kuwa unayo akiba ya mafuta ya taa ya kutosha, vioo, utambi n.k. Taa moja hutumia debe moja la mafuta ya taa kwa muda wa siku 16 hadi 20. Unashauriwa uweke mafuta kwenye taa asubuhi na kukagua jioni kama yanatosha kwa sababu taa ikizimika
usiku utapata hasara ya vifo kwa vifaranga kujikusanya na kukosa hewa .Weka mafuta ya
kutosha lakini usijaze taa. Joto la taa za chemli hurekebisha kwa kupandisha au kushusha utambi pia kuongeza au kupunguza idadi ya taa.

3. Jiko la Mkaa
Jiko la mkaa linaweza kutumika badala ya taa kwa ajili ya kuwapa vifaranga joto. Unapotumia jiko la mkaa ni hakikisha kwamba mkaa unaotumia hautoi moshi na chumba kinapitisha hewa safi na ya kutosha. Pia jiko liwekwe juu ya matofaili ili kuzuia vifaranga wasiliguse.

4. Mwamvuli
Mfugaji akimudu anaweza kutengeneza mwamvuli wa kuning’inia juu ya kitalu cha kulea vifaranga kwa kutumia makaratasi magumu ya “hardboard”. Mwamvuli unasaidia kupunguzaupotevu wa joto na hivyo kupunguza matumizi ya mafuta ya taa. Kwenye mwamvuli wa duara toboa tundu moja ili kupitisha hewa yenye joto. Angalia mviringo wa mwamvuli wako uwiane na ukubwa wa kitalu chako. Ili kuwapa vifaranga uhuru wa kufuata au kuepuka joto. Ni lazima mwamvuli uwekwe juu ya matofali na kila juma inabidi uinuliwe juu kiasi cha cm 5 (inchi 2, kufuatana na hali ya hewa.
5. Vyombo vya chakula (Vihori)
Ili vifaranga wakue vizuri vyombo vya chakula lazima viwafae. Vipimo pamoja na idadi ya vyombo vya chakula ni vya muhimu viwatosheleze. Chombo chenye urefu wa (futi 3 x inch 3) kinatosha vifaranga 100. Ukitumia mbao kutengeneza vyombo vya chakula unashauriwa mbao ziwe unene wa cm 1/25 (inchi ½). Pia, unaweza kutumia sahani za kawaida unazotumia nyumbani kuwawekea vifaranga chakula. Chombo cha kulishia vifaranga

6. Vyombo vya maji:
Chombo chochote chenye kina kifupi kinafaa kwa kuwayweshea kuku ila budi kiinuliwe ili vifaranga wasiweze kuingiza takataka za chini kwenye maji. Pia kama ni cha wazi maji yawekewe changarawe safi kabisa ili kuzuia vifaranga wasiloane maji. Au tumia sahani na makopokama ifuatavyo. Toboa sentimita tatu kutoka kwenye mdomo wa kopo, jaza maji katika kopo halafu lifunike kwa sahani na ligeuze. Kinywesheo cha vifaranga

Maandalizi kabla na matunzo baada ya kupokea vifaranga
Maandalizi kabla ya kupokea vifaranga
Inashauriwa vifaranga walelewe katika chumba maalum hadi umri wa majuma manne. Chumba kitayarishwe siku kumi na nne kabla ya vifaranga kuwasili kama ifuatavyo:
• Matundu yote yaliyo kwenye sakafu, dari, madirisha na ukuta yazibwe.
• Kama chumba hicho kina sakafu ya saruji, kisafi shwe kwa maji ya moto na baadaye kinyunyizie dawa kama vile Rhino au Dettol ya kuua wadudu. Ikiwa chumba hicho hakina sakafu ya saruji, toa takataka zote kisha mwagia chokaa au majivu.
• Mazingira ya nje ya banda yawekwe katika hali ya usafi ili kuzuia wadudu waharibifu. Kusafi shwe hadi kufi kia upana wa mita mbili au zaidi kuzunguka banda.
• Katika chu  na umbile la duara, itengenezwe kwakutumia karatasi ngumu au majamvi. Mduara huhifadhi joto, huzuia upepo na huzuia vifaranga wasiende mbali na chanzo cha joto.
• Sakafu iwekwe matandazo yaliyopigwa dawa mfano ya kuuwa wadudu kama Municipal disinfectant. Matandazo yaweza kuwa pumba ya mpunga, maranda ya mbao, nyasi, mchanga, maganda ya karanga n.k. Masaa mawili kabla ya kuwasili vifaranga vyenye umri wa siku moja taa au jiko liwashwe kwenye chumba cha kulelea vifaranga. Hii itasaidia ili maji na chumba kuanza kupata joto la kutosha kuwawezesha vifaranga kula, kunywa bila shida. Baada ya masaa mawili kupita ndipo chakula kianze kuwekwa kwenye vyombo vya chakulana vifaranga waanze kula.

Matunzo baada ya kupokea vifaranga Kuwapa joto
Mfugaji anaweza kulea vifaranga wengi kwa kutumia Kitalu (mduara) unaoweza kutengenezwa
kwa kutumia mbao au karatasi ngumu. Au kwenye pembe moja ya chumba ambapo utawaweka vifaranga zungusha vifaa vya kutunza na kuongeza joto . Vifaranga hujikusanya karibu nachanzo cha joto kama taa au jiko kujilundika katika sehemu moja kama joto ni kidogo. Hivyo ongeza joto kwa kushusha taa chini na kama bado joto litakuwa halitoshi, ongeza vifaa vya joto kama taa ya pili kutegemeana na hali halisi.
Mfano wa brooder kwaajili ya kutunzia vifaranga


 Kama joto halitoshelezi utaona yafuatayo
Vifaranga wakiona baridi , hujikusanya karibu zaidi na chanzo cha joto. au wao wenyewe hujikusanya pamoja kwenye pembe ya kitalu au nyumba na hulia kwa sauti. Ukiona hivi ongeza kiwango cha joto adi waonekane kutawanyika kote kitaluni.
Katika mduara/ kitalu cha kulea vifaranga mfugaji anatakiwa kufuatilia na kutambua kama hali ya joto iliyopo inawafaa vifaranga au la. Ufuatiliaji wa karibu utamsaidia kuchukua hatua mapema endapo marekebisho yatahitajika. Hii utafahamu kwa kuangalia tabia ya vifaranga wanapokuwa ndani ya kitalu .

Kama joto linatosheleza utaona yafuatayo
• Vifaranga vitalia kwa furaha,
• Vitakimbia kimbia,
• Vitakunywa maji,
• Vitachaguachagua takataka na
• Kuonyesha shughuli nyingi, zote hizi ni dalili nzuri kuwa joto linatosha.
Mfano wa kitunza joto kwa vifaranga

Kama joto likizidi utaona yafuatayo
• Vifaranga wakikaa mbali na vifaa vya joto nidalili kuwa joto limezidi.
• Joto likiwa kali vifaranga hukimbia kutoka kwenye mwamvuli (kama umewekwa).
• Husinzia na huzubaa. Katika hali hii itabidi upunguze joto kwa kupandisha taa juu na kama bado joto ni kali punguza vifaa vya joto na kuwapa vifaranga maji mengi ya kunywa.




Kama kutakuwa na upepo unaopuliza kutoka upande mmoja utaona yafuatayo
Vifaranga watajikusanya upande mmoja wa kitalu mbali na upepo unakotokea. Kutegemeana na jinsi utakavyowaona vifaranga wanafanya, kama wataashiria tatizo, fanya marekebisho mapema kabla hayajatokea madhara kwa vifaranga.

Katika majuma 5 ya kwanza vifaranga huhitaji joto usiku na mchana na
katika majuma 3 yanayofuata joto hujitajiwa wakati wa usiku tu.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa joto katika nyumba ya vifaranga hubadilika kufuata maeneo tofauti na pia kutegemeana na majira tofauti ya mwaka. Hivyo kama hali ya baridi ikizidi, muda wa kuwasha taa urefushwe, wakati wa joto kali taa zinaweza kuzimishwa hata kama ni juma la kwanza au la pili. Jambo la msingi ni mfugaji kuwa macho na kuwapa vifaranga joto la kutosha mara tu hali ya hewa ikibadilika kuwa ya baridi ghafla.
Hali ya hewa ikiwa nzuri madirisha yafunguliwe katika juma la kwanza au la pili kwa ajili ya kutunza matandazo sakafuni yasiwe na unyevu. Vifaranga huota manyoya mapya wakiwa na umri wa majuma 5 – 6 lakini huotesha manyoya ya kutosha katika juma la 8. Wakiisha ota manyoya ya kutosha vifaranga wanaweza kuvumilia zaidi hali ya baridi. Ufuatiliaji wa karibu ni muhimu kwa kipindi chote cha majuma matano (5) ili kuepusha vifo visivyokuwa vya lazima.

Waondoe vifaranga kwenye kitalu cha kuwalea mara tu wakiwa na manyoya ya kutosha, yaani katika juma la 4 -5 kutegemeana na hali yao ya manyoya na hali ya hewa iliyopo.
Ulishaji wa Vifaranga
Chakula na Maji
Ili vifaranga wawe na maendeleo mazuri ya ukuaji, wanatakiwa wapewe chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini ambavyo ni Protini, Madini, Wanga na Vitamin pamoja na maji safi wakati wote.
• Pia chakula kunaweza kuchanganywa na mchanga kidogo ambao husaidia usagishaji wa chakula kilicholiwa.
• Hakikisha vyombo vya maji vinakuwa safi wakati wote.
• Chakula na maji yabadilishwe kila baada ya masaa 24.
• Hakikisha vifaranga wanapewa chakula wanachoweza kumaliza katika masaa 24 ili kuzuia uharibifu. Siku 7 – 10 baada ya kupokea vifaranga vyombo vya mwanzo vya maji na chakula vibadilishwe wawekewevyombo vya kawaida. Vifaranga wapewe maji safi , vyombo vya maji visafi shwe na kujazwa maji mara mbili kila siku. Kila asubuhi sehemu zilizo na vyombo vya maji zikaguliwe na takataka zenye unyevu ziondolewe.
Vyombo vya chakula vijazwe nusu hasa vifaranga wakiwa na umri wa siku 10 – 14. Pia vifaranga wakiwa na umri huo huo wapewe majani mabichi yaliyo bora na yenye thamani. Majani yafungwe mafungu na kuning’inizwa kwa kamba.

Vyombo vya chakula na maji
Vyombo vya chakula na maji vinaweza kuwa ni makopo, sufuria, karai n.k. Pia vinaweza kuundwa kwa kukata madebe, galoni za plastiki, vibuyu n.k. Aidha vyombo hivyo vinaweza kutengenezwa kwa kutumia mbao, mianzi, Jambo la muhimu ni kuhakikisha kuwa vyombo hivyo haviruhusu kuku kuchafua chakula au maji. Mfano wa vyombo vya chakula na maji ambavyo mfugaji anaweza kujitengenezea.Mfano wa kilishio Vifaranga wakiwa bado wadogo anaweza kutumia sahani za chakula kuweka kokoto safi na
kuzitumia kunyweshea vifaranga maji.
Aina ya vyakula Kiasi                                                      ( Kilo)
Nafaka kama mahindi au mtama                                              40
Pumba za mtama, mahindi, uwele,                             27
Mashudu ya, alizeti, ufuta, karanga, au soya              20
Unga wa mifupa, chokaa                                                          2.25
Dagaa au mabaki ya samaki                                        10
Chumvi ya jikoni                                                         0.5
Virutubisho (Premix)                                                               0.25
Jumla                                                                          100
Mfano wa mchanganyiko wa chakula cha vifaranga
Mwavuli:
Kama uliweka mwavuli kwenye kitalu uinue juu kiasi cha fi ti 1 kila juma. Unaweza kuondoa
mduara vifaranga wakiwa na umri wa majuma 4 – 5. Lakini mwamvuli usiondolewe mpaka
vifaranga viote manyoya ya kutosha.
Vichanja:
Vifaranga vipewe vichanja ili vizoee kupanda na kulala juu, vikiwa na umri wa majuma 4.
Chanjo na tiba ya Magonjwa
Ni wazi kuwa hatari kubwa inayokabili vifaranga ni magonjwa. Yapo maradhi mengi ya
vifaranga. Hata hivyo itakuwa vigumu kuyaelezea maradhi yote hapa. Kitakachoelezwa
katika mwongozo huu ni magonjwa yanayosumbua mara kwa mara kwenye ukanda wa kati
wa nchi hii. Ukipata shida tofauti na zinazoelezwa hapa tafadhali mwendee Bwana Mganga
wa mifugo aliye karibu akusauidie.

Kinga dhidi ya magonjwa
Ni muhimu sana vifaranga kupewa kinga dhidi ya magonjwa mbali mbali yanayotokea katika eneo husika. Kinga nyingi hutolewa kwa njiaa ya chanjo hasa kwa magonjwa yasiyotibika kama tutakavyoona katika maelezo yafuatayo.

Chanjo muhimu kwa vifaranga
Kwa magonjwa yanayosababishwa na virusi
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Mdondo
Ø  Vifo vingi vya ghafla kwenye kundi hadi 90% -100%.
Ø  Kizunguzungu, kupinda shingo, kutembea kinyume nyume, kupooza mabawa,kuanguka chali, kupoteza fahamu na hatmaye kufa.
Ø  Kupoteza fahamu ya kula, kuzubaa, kusinzia,kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani kibichi na baadaye kufa.
Ø  Hakuna tiba.
Ø  Kinga: chanja kwa kutumia chanjo ya kideri vifaranga wakiwa na umri wa siku tatu na rudia baada ya wiki tatu na kila baada ya miezi mitatu.
Ø  Hakikisha usafi wa banda na vyombo.
Ø  Kutenga vifaranga wanaoumwa
Ø  Tenga vifaranga wagenikwa muda wa wiki mbili na kuwachanja kabla ya kuwachanganya na vifaranga wenyeji.


Ndui ya kuku
Ø  Vipele vya mviringo ambavyo huweza kuungana na kusababisha vidonda kwenye upanga, masikio na miguu hususan sehemu zisizo na manyonya.
Ø  Utando mweupe mdomoni.
Ø  Vifo hutokea kwenye vifaranga.
Ø  Hakuna tiba
Ø  Kinga: wachanje kuku wakiwa na umri wa miezi miwili kwa kutumia chanjo ya ndui.
Ø  Zingatia usafi wa banda wakati wote.
Ø  Watenge kuku wagonjwa ili wasiwaambukize wengine.Gomboro
Ø  Viranga wa umri wa wiki tatu hadi sita.
Ø  Idadi ya kuku waliopatwa na ugonjwa katika kundi huwa kubwa.
Ø  Huharisha kinyesi cha maji maji.
Ø  Hushindwa kusimama.
Ø  Manyoya husimama, hutetemeka na hatimaye hufa.

Kinga:
Ø  chanja vifaranga wakiwa na umri wa siku rudia kuchanja baada siku 21.
Tiba ya Magonjwa kwa vifaranga
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Homa ya matumbo(Fowl typhoid), Kuzubaa, kuvimba viungo vya miguu, kuchechemea, kukosa hamu ya kula, kuharisha kinyesi chenye rangi ya njano au kijani hatimaye kufa.
Ø  Kuku wageni watengwe na kufanyiwa uchunguzi wa damu kabla ya kuchanganywa kwenye kundi.
Ø  Kufanya uchunguzi wa damu mara kwa mara ili kubaini kuku wenye vimelea vya ugonjwa na
kuwaondoa.
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Mdondo Vifo vingi vya ghafla
kwenye kundi hadi 90% -100%.
Ø  Kizunguzungu, kupinda shingo, kutembea kinyume nyume, kupooza mabawa, kuanguka chali, kupoteza fahamu na hatmaye kufa.
Ø  Kupoteza fahamu ya kula, kuzubaa, kusinzia, kuharisha kinyesi chenye rangi ya kijani kibichi na baadaye kufa. tiba. chanja kwa kutumia chanjo ya kideri vifaranga wakiwa na umri wa siku tatu na rudia baada ya wiki tatu na kila baada ya miezi mitatu.
Ø  Hakikisha usafi wa banda na vyombo.
Ø  Kutenga vifaranga wanaoumwa
Ø  Tenga vifaranga wageni kwa muda wa wiki mbili na kuwachanja kabla ya kuwachanganya na vifaranga wenyeji.
Mafua kuku (Infectious coryza)
Ø  Kutoa machozi.
Ø  Kuvimba macho na hatimaye hutoa usaha wenye harufu mbaya.
Ø  Kupiga chafya na kukohoa.
Ø  Kutokwa na ute kwenye pua na mdomo ambao hatimaye hugeuka na kuwa makamasi mazito.
Ø  Kupumua kwa shida na kutoa saudit ya kukoroma.
Ø  Kushindwa kula
Ø  Kudhoofika na hatimaye anaweza kufa.
Tiba:
 ugonjwa unatibika kama hatua za kudhibiti zitachukuliwa mapema. Muone mtaalamu wa mifugo kwa ushauri wa aina ya dawa ya kutumia.

Ugonjwa unayosababishwa na Protozoa
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Kuharisha damu (Coccidiosis)
Ø  Kuzubaa
Ø  Kushusha mabawa kama mtu aliyevaa koti.
Ø  Kupoteza hamu ya kula.
Ø  Kuharisha kinyesi chenye rangi ya kahawia au kilichochanganyika nadamu.
Ø  Kuharisha damu
Ø  Manyoya kutimka
Ø  Kupauka kwa upanga na ndevu
Ø  Kudhoofika na hatimaye huweza kufa.
Tiba:
Ugonjwa huo unaweza kutibika kwa amprolium, salfa na ESb3 kama hatua za kuudhibiti zitachukuliwa mapema.Kinga kuepuka unyevunyevu katika matandiko. Kuwatenga kuku
wanaoonyesha dalili za ugonjwa. Kinga kwa kutumia coccidiostat. Kutibu kwa kufuata ushauri
wa wataalam wa mifugo.
Ø  Hushindwa kusimama.
Ø  Manyoya husimama, hutetemeka na hatimaye hufa
.
Tiba ya Magonjwa kwa vifaranga
Ugonjwa Dalili za Ugonjwa Kinga/Tiba
Homa ya matumbo(Fowl typhoid) Kuzubaa, kuvimba viungo vya miguu, kuchechemea, kukosa hamu ya kula, kuharisha kinyesi chenye rangi ya njano au kijani hatimaye kufa.
Ø  Kuku wageni watengwe na kufanyiwa uchunguzi wa damu kabla ya kuchanganywa kwenye kundi.
Ø  Kufanya uchunguzi wa damu mara kwa mara ili kubaini kuku wenye vimelea vya ugonjwa na kuwaondoa.

Athari zinazosababishwa na wadudu wanaonyonya damuKisababishi Dalili za athari za
Wadudu

Kinga/Tiba
Utitiri na viroboto
Ø  Kujikuna na kujikung’uta.
Ø  Kunyonyoka manyoya,
Ø  Kupauka macho, upanga, ndevu na masikio.



Tiba:
Wadudu wanaweza kudhibitiwa kwa kunyunyizia dawa kuku walioshambuliwa.
Kinga:
Ø  Kuzingatia usafi wa mabanda ndani na nje.
Ø  Kunyunyizia dawa za kuua wadudu kwenye viota pamoja na kuku anayetaka kuatamia.
Ø  Kuchoma au kufukia mayai ambayo hayakuanguliwa pamoja na maganda ya mayai.

Athari za Upungufu wa virutubishi kwenye chakula Kisababishi Dalili za athari za Wadudu
Kinga/Tiba
Upungufu wa virutubisho Kudumaa
Tiba:
Athari zinazotokana na upungufu wa virutubisho zinaweza kurekebishwa kwa kuwapa vifaranga virutubisho vilivyopungua katika chakula.
Kinga:
Kuwalisha chakula kilicho na mchanganyiko wenye uwiano sahihi katika wanga, protini, vitamin, madini na maji ya kutosha.

Kumbukumbu ya kutibu vifaranga kwa kipindi cha wiki 5 tangu kutotolewa
Tarehe Na Mwezi
Ugonjwa Aina na kiasi cha chanjo Matibabu Gharama Maoni

Kumbukumbu muhimu wakati wa kukuza vifaranga
Kumbukumbu ya vifaranga kwa kila Mwezi….. Mei…..
Tarehe Idadi ya vifaranga Kiasi cha chakula kilichotumiwa
Vifo Vifaranga vilivyo ondolewa
Vifaranga vya wiki 5
vilivyouzwana bei yake.
                                                            
                                                        Cypranoanimalfarms.blogspot.com

Category